• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yawapatia wanafunzi 30 wa chuo kikuu wa Uganda udhamini wa masomo

    (GMT+08:00) 2018-08-09 09:17:17

    China imetoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi 30 wa Uganda wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini humo.

    Balozi wa China nchini Uganda Bw Zheng Zhuqiang amesema kuna hitaji la haraka la kuwekeza kwenye sekta ya rasilimali watu nchini Uganda, ili kuhimiza ongezeko na mageuzi yaliyopangwa.

    Ameongeza kuwa udhamini wa masomo kutoka ubalozi wa China utatolewa kila mwaka kwa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Makerere. Zaidi ya hayo, serikali ya China inawapatia wanafunzi zaidi ya 500 wa Uganda udhamini wa masomo ili kuja China kwa ajili ya masomo. Na maofisa 600 wa serikali ya Uganda pia wamepata fursa ya kupata mafunzo ya muda mfupi nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako