• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nini kiko nyuma ya hatua ya Marekani kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 1.6 za kimarekani kutoka China?

    (GMT+08:00) 2018-08-09 09:24:15

    Baada ya Marekani Julai 6 kuongeza ushuru wa asilimia 25 dhidi ya bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 3.4 za kimarekani kutoka China, ofisi ya mjumbe wa biashara wa nchi hiyo juzi ilitangaza tena orodha ya bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 1.6 kutoka China zitakazoongezewa ushuru wa asilimia 25 tangu Agosti 23.

    Sababu moja inayotajwa na Marekani kuanzisha vita ya biashara ni kufikiria usalama wa taifa wa Marekani, na kurejesha nguvu za kiviwanda nchini humo ili kutoa nafasi zaidi za ajira kwa wamarekani. Lakini matokeo yamekuwa tofauti.

    Kampuni ya Element Electronics ya Marekani tarehe 6 ilitangaza kuwa litafunga kiwanda cha televisheni huko South Carolina baada ya miezi miwili kutokana na ongezeko la gharama linalotokana na serikali ya Marekani kuongeza ushuru dhidi ya vifaa vinavyotoka China. Takwimu kutoka taasisi ya uchumi wa kimataifa ya Peterson zinaonesha kuwa, kama Marekani ikitoza ushuru wa asilimia 25 dhidi ya magari kutoka sehemu nyingine duniani, wafanyakazi laki 2 hivi wa nchi hiyo watapoteza ajira ndani ya mwaka mmoja hadi mitatu. Kama nchi nyingine zitachukua hatua ya kulipiza kisasi, Marekani itapoteza nafasi laki 6.24 hivi za ajira.

    Benki ya Atlanta ya Marekani imefanya uchunguzi ukionesha kuwa, wasiwasi kuhusu ushuru unazilazimisha moja kwa tano ya kampuni za Marekani kutathmini tena, kuahirisha au kuacha mipango ya uwekezaji. Benki hiyo pia imesema, athari zinazoletwa na mvutano wa kibiashara kwa kampuni za Marekani ziko katika sekta ya viwanda, kama hali hiyo ikiendelea kupamba moto, athari hiyo mbaya kwa uwekezaji wa kampuni za Marekani inaweza kuongezeka.

    Ni dhahiri kwamba fimbo ya ushuru inayotumiwa na serikali ya Marekani inaichapa Marekani yenyewe na raia wake. Sauti ya kupinga ongezeko la ushuru inaendelea kuongezeka, serikali ya Marekani inatakiwa kufanya mambo yanayoendana na maslahi ya watu wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako