• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AMISOM yawataka washirika wake kuongeza operesheni dhidi ya kundi la Al Shabaab

  (GMT+08:00) 2018-08-09 18:40:31

  Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kimeutaka Umoja huo na askari wa jeshi la Somalia kuongeza operesheni za pamoja za usalama ili kuwaondoa wapiganaji wa Al Shabaab nchini humo.

  Kamanda wa Kikosi hicho Jim Meesigye Owoyesigire amewataka askari wake katika mkoa wa Hirshabelle kuongeza uratibu na askari wa jeshi la Somalia ili kuboresha amani na usalama. Kamanda huyo amesifu juhudi na nia ya vikosi vya AMISOM katika kuleta amani mkoani humo.

  Mashirika ya misaada yamesema hali mbaya ya barabara katika sehemu ya kusini katikati mwa Somalia kumetoa mazingira kwa wapiganaji wa kundi la Al Shabaab kuendelea kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kutumia vifaa vya mlipuko dhidi ya misafara ya AMISOM na vikosi vya usalama vya Somalia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako