• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Zimbabwe yajiandaa kumwapisha Mnangagwa licha ya tishio la kufunguliwa kesi

    (GMT+08:00) 2018-08-09 18:40:48

    Serikali ya Zimbabwe imepanga kumwapisha rais mteule Emmerson Mnangagwa jumapili ijayo, licha ya tishio lililotolewa na muungano wa upinzani wa MDC kuonyesha nia ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Julai 30 mahakamani.

    Muungano wa MDC umeonesha nia ya kupinga ushindi wa rais mteule Mnangagwa mahakamani, pia umesema utapinga matokeo katika majimbo 20 ambayo chama cha ZANU-PF kimeshinda.

    Sheria nchini Zimbabwe inaelekeza kuwa mtu anayeshinda uchaguzi wa rais anapaswa kuapishwa siku ya tisa baada ya matokeo rasmi kutangazwa, isipokuwa kama kuna mgombea yoyote anayepinga matokeo hayo, na anatakiwa kufungua kesi ndani ya siku saba tangu kutangazwa kwa matokeo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako