• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatua za Marekani huenda zitakwamisha ukuaji wa uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2018-08-09 18:44:42

    Mei 8 mwaka huu, serikali ya Marekani ilitangaza kujitoa kwenye makuabaliano ya nyuklia ya Iran JCPOA yaliyofikiwa mwaka 2015, na kurejesha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran.

    Vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran vinahusisha sekta za nishati, mafuta na fedha, wakati sekta ya mafuta, ambayo ni nguzo muhimu ya uchumi wa Iran, inachangia asilimia 70 hadi 80 ya pato la Iran. Vikwazo hivyo vitasababisha kupanda bei ya mafuta duniani kwa kuwa Iran ikiwa ni nchi ya nne kwa uzalishaji mkubwa wa mafuta duniani, Marekani pia imetishia kuwa haitafanya biashara na nchi yoyote inayoendelea na biashara na Iran.

    Hatua nyingine ni vita ya kibiashara iliyoanzishwa na Marekani, na ingawa rais Trump amesema kuwa Marekani inashinda vita hiyo, wachambuzi wanaona kuwa sera zake za ushuru si kama tu zitayumbisha imani ya biashara, bali pia zitaweza kukwamisha ukuaji wa uchumi na kusababisha mfumuko wa bei kote duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako