• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jack Ma kuwasaidia wajasiriamali vijana wa Afrika

  (GMT+08:00) 2018-08-09 19:02:27

  Mfanyabiashara maarufu wa China ambaye ni muasisi wa biashara ya mtandao wa Alibaba Bw Jack Ma jana jijini Kigali alizindua tuzo ya ujasiriamali wa mitandaoni (Netpreneur Prize) ili kuwaunga mkono viongozi wa biashara barani Afrika.

  Tuzo hiyo ilizinduliwa katika kongamano lililopewa jina la :Wajasiriamali:Uibukaji wa Simba wa mitandao Afrika.

  Tuzo itawazawidi wajasiriamali 100 wa Afrika dola za kimarekani 10 milioni katika kipindi cha miaka 10 ikilenga uvumbuzi wa mashinani,uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake na biashara ndogo.

  Jack Ma alisema kama mjasiriamali anaelewa umuhimu wa kupata msaada nyakati za mwanzo.Alisema tuzo hiyo inaonyesha msaada wao kwa kizazi kijacho cha wajasiriamali barani Afrika ambao wanafungua njia kwa ajili ya maisha bora siku zijazo na kufanya mabadiliko chanya katika jamii zao.

  Ma anasema ameanzisha mpango huo baada ya kuvutiwa na uwezo wa ujasiriamali wa vijana aliokutana nao baada ya kuzuru Afrika kwa mara ya kwanza mwaka jana.

  Jack Ma aliwahimiza vijana kuota ndoto kubwa na kuwa na ubunifu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako