• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shughuli za biashara zarejea mji wa mpakani wa Namanga

  (GMT+08:00) 2018-08-09 19:04:29

  Shughuli za kibiashara zimeanza kurudi katika hali ya kawaida katika mji wa Namanga unaopakana na nchi ya Tanzania baada ya kukatizwa kwa siku tatu kufuatia madai ya wafanya biashara wa Kenya kudai kuangaishwa na uongozi wa Tanzania.

  Hii ni baada ya kamati ya kusimamia mipaka nchini Kenya kufanya mkutano wa dharura katika mpaka huo kutatua tatizo hilo.Kamati hiyo inajumuisha maofisa kutoka shirika la forodha la, shirika la kukadiria ubora wa bidhaa na asasi zingine za serikali mpakani.

  Kamati hiyo imekubalia kuyashughulikia masuala yaliyowasilishwa na waafanya biashara wa Kenya na kutoa ripoti kamili baada ya wiki moja.Ghasia hizo zimewasababishia wafanya biashara hao hasara ya mamilioni ya fedha.

  Tanzania pia huwa na halmashauri ya kusimamia shughuli za mpaka huo na pande zote mbili hukutana kila baada ya robo ya mwaka .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako