• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bei ya kuku Dar es Salaam yaongezeka huku usambazaji ukipungua

  (GMT+08:00) 2018-08-09 19:06:52

  Jiji la Dar es Salaam hivi sasa linashuhudia uhaba wa kuku ,jambo lililosababisha kuongezeka kwa bei.

  Utafiti uliofanywa katika masoko kadhaa jijini humo ikiwa ni pamoja na Kisutu,Tegeta,Ilala na Shekilango umeonyesha kuwa bei za rejareja za kuku zimeongezeka kwa takriban asilimia 40 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

  Wakati wa utafiti huo ilibainishwa kuwa bei za rejareja za kuku zilipanda hadi Sh7,000 na Sh8,000 mwanzoni mwa wiki hii kutoka bei ya wastani ya Sh6,000 katikati mwa mwezi Mei kulingana na uzito wa kuku.

  Bei za jumla pia zimeongezeka hadi wastani wa Sh7,500 kwa kuku mmoja kutoa bei ya Sh5,500.

  Wauzaji jumla wamesema kupanda kwa bei ya kuku ni kutokana na usambazaji mdogo usioweza kukidhi mahitaji,pamoja na kupanda kwa gharama za ufugaji kuku.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako