• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya-Wenye magari wataka barabara kupanuliwa Mombasa

  (GMT+08:00) 2018-08-09 19:07:38

  Wamiliki wa magari ya abiria mjini Mombasa wametoa wito wa kupanuliwa kwa barabara za katikati ya mji ili kuzuia msongamano wa magari.

  Mshirikishi wa chama cha wamiliki wa matatu mjini humo Bw Salim Mbarak amesema barabara hizo zinatakiwa kupanuliwa haraka ili kurahisisha biashara ya usafiri.

  Ameongeza kuwa baadhi ya barabara zimeharibika jambo ambalo linasababisha msongamano mkubwa wa magari hali ambayo inapunguza mapato yao ya kibiashara.

  Wito huo unakuja miaka miwili tu baada ya idara ya trafiki ya kaunti ya Mombasa kupunguza mizunguko miwili mikubwa ya barabara katikati ya mji huo kwa ajili ya kupunguza msongamano katika barabara ya Digo.

  Miaka ya hivi karibuni mji wa Mombasa umeonekana kujivunia zaidi hali ya miundo mbinu kufuatia miradi mbali mbali ya kuboresha usafiri ikiwemo ujenzi wa reli ya SGR na kufunguliwa kwa awamu ya kwanza ya barabara ya Dongo Kundu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako