• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yaonya kuIwekea Russia vikwazo vikali zaidi

    (GMT+08:00) 2018-08-09 19:31:50

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Heather Nauert jana amesema, Marekani imethibitisha kuwa serikali ya Russia imekiuka sheria ya kimataifa katika tukio la jasusi wa zamani wa Russia kuwekewa sumu ya neva, na imeamua kuiwekea Russia vikwazo, ambavyo huenda vitakuwa vikali zaidi kwa mujibu wa hali inayoendelea.

    Amesema, vikwazo vipya vitatekelezwa kuanzia tarehe 22 Agosti, lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusu maudhui ya vikwazo hivyo.

    Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Russia nchini Marekani inasema, vikwazo vipya vya Marekani ni vikali sana, na msimamo wa serikali ya Russia wa kufanya uchunguzi wa wazi na haki na kuadhabu wahalifu haujabadilika. Ubalozi huo umeitaka serikali ya Marekani pia ifuate msimamo huo na kuuweka wazi uchunguzi wake kuhusu tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako