• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchaguzi chama cha kuogolea kufanyika Agosti 26

  (GMT+08:00) 2018-08-10 08:20:00
  Baraza la Michezo la Taifa nchini Tanzania (BMT), limetangaza tarehe ya uchaguzi wa Chama cha Kuogelea nchini (TSA) kufanyika Agosti 26, mwaka huu.

  Akizungumza na Azam Sports, Afisa Habari wa BMT, Frank Mgunga amesema nafasi zitakazogombewa ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Mweka Hazina, Mkurugenzi wa Ufundi na Mkurugenzi wa Elimu na Maendeleo.

  Frank amesema usaili wa wagombea utafanyika tarehe 25 Agosti, 2018 ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi na fomu za kugombea zinapatikana kwa shilingi 100,000 kwa kila nafasi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako