• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ndondi: Campbell kurudiana na Mendy

  (GMT+08:00) 2018-08-10 08:20:55
  Bondia Luke Campbell wa Uingereza amepata nafasi ya kuuthibitishia ulimwengu madai yake kuwa alipoteza pambano dhidi ya Yvan Mendy kwa kudhulumiwa.

  Campbell alishindwa kwa pointi katika pambano hilo lililofanyika mwaka 2015 lakini alipinga kushindwa huku akidai katika pambano hilo kuwa yeye ndio alistahili kushinda.

  Campbell bingwa wa Olimpiki uzani wa Light atapanda uliongoni Septemba 22 mwaka huu kuzipiga katika pambano la kuwania ubingwa wa WBC kwenye uwanja wa Wembley.

  Pambano hilo litakuwa ni la utangulizi kabla ya pambano la ubingwa wa dunia uzito wa juu wa WBC kati ya Anthony Joshua wa Uingereza na Alexander Povetkin wa Urusi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako