• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Dirisha la uhamisho wa wachezaji lafungwa jana nchini Uingereza

  (GMT+08:00) 2018-08-10 08:21:13
  Dirisha la uhamisho wa wachezaji katika majira ya joto limefungwa jana nchini Uingereza huku Chelsea ikiwa imeweka rekodi ya uhamisho ghali zaidi wa golikipa.

  Ada ya Euro milioni 71 kwa golikipa Kepa Arrizabalaga ktoka klabu ya Athletic Bilbao ya Hispania, usajili huo umekuja baada ya Chelsea kuondokewa na kipa wake Thibaut Courtois aliyejiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa ada ya Euro milioni 35.

  Liverpool ilimsajili kipa Allison kutoka AS Roma kwa ada ya Euro milioni 66.

  Manchester United inahaha kusaka wachezaji nyota kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili na ripoti za hivi punde zinasema inazungumza na beki wa Atletico Madrid Diego Godin ili kumpeleka Old Trafford.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako