• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AFCON 2019: Maandalizi yanaendelea vizuri

  (GMT+08:00) 2018-08-10 08:22:37

  Serikali ya Tanzania imesema maandalizi ya kuandaa michuano ya soka ya vijana ya Kombe la Afrika chini ya miaka 17 AFCON 2019 yanakwenda vizuri kwa kuhakikisha michuano hiyo itafanyika kwa uhakika mwakani.

  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Suzan Mlawi alipokuwa katika kikao na Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo pamoja na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF.

  Michuano hiyo ya vijana ya AFCON imepangwa kuchezwa katika viwanja vitatu vya Taifa, Uhuru na Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.

  Hata hivyo wasimamizi wa michuano hiyo Shirikisho la Soka la Afrika CAF, limeagiza Uwanja wa Uhuru ufanyiwe ukarabati ambao unagharimu shilingi bilioni 1.6.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako