• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iraq yatangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa wabunge baada ya kurudia kuhesabu kura

    (GMT+08:00) 2018-08-10 09:32:10

    Tume ya uchaguzi ya Iraq imetangaza matokeo ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika Mei 12 kukiwa na mabadiliko kidogo. Taarifa iliyotolewa na jopo la majaji 9, waliochukua nafasi ya wajumbe wa tume ya uchaguzi kwenye kazi ya kuhesabu upya kura, imesema hakuna mabadiliko katika majimbo 13 kati ya 18, kuna mabadiliko kwa washindi wa viti vitano lakini ndani ya muungano ya vyama.

    Mabadiliko makubwa yametokea katika eneo la Baghdad, ambapo muungano mmoja umepata kiti kimoja zaidi, na mwingine kiti chake kimoja kimepungua.

    Habari pia zinasema kiongozi wa kundi la washia Bw. Moqtada al Sadr ametishia kurudi kwenye upinzani kama masharti 40 aliyoweka kwa waziri mkuu ajaye wa Iraq hayajatimizwa. Baadhi ya masharti aliyojata ni kuwa waziri mkuu ajaye asiwe na uhusiano na chama chochote cha siasa, na asiwe mbunge. Pia hatakiwi kuwa mshukiwa wa ufisadi, au kuwa na uraia wa nchi mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako