• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM afuatilia kurudishwa kwa nguvu kwa kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe kutoka Zambia

    (GMT+08:00) 2018-08-10 09:32:42

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema anafuatilia kwa tahadhari tukio lililotokea jana nchini Zimbabwe, kufuatia kurudishwa kwa nguvu kwa kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Bw. Tendai Biti kutoka Zambia.

    Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq, amesema kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuwa wanafuatilia hali ya tukio la Bw. Biti kukataliwa hifadhi na kurudishwa nyumbani nchini Zimbabwe.

    Bw. Biti alikimbia Zimbabwe wakati polisi wanamtafuta kwa tuhuma za kuchochea vurugu za wiki iliyopita, baada ya chama cha ZANU-PF kutangazwa mshindi.

    Bw. Haq amesema Shirika la Kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linafuatilia kurudishwa kwa nguvu kwa Bw. Biti, kitendo ambacho ni kinyume na sheria ya kimataifa ya wakimbizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako