• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hamas na Israel zakubaliana kusimamisha mapambano ukanda wa Gaza

  (GMT+08:00) 2018-08-10 09:35:49

  Kundi la Hamas limetangaza kufikia makubaliano na Israel kuhusu kusimamisha mapambano yanayopamba moto katika ukanda wa Gaza.

  Makubaliano hayo yaliyopatanishwa na Misri na mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati Bw. Nickolay Mladenov, yatamaliza duru nyingine ya makabiliano ya kijeshi kati ya Israel na kundi la Hamas.

  Ndege za kivita za Israel zimeshambulia vituo zaidi ya 150 huko Gaza tangu jumatano usiku, na kusababisha kifo cha mjamzito, mtoto wake na mpiganaji wa Hamas. Wakati huohuo, wapiganaji wa Gaza wamerusha maroketi zaidi ya 100 dhidi ya eneo la kusini mwa Israel, ambayo yamesababisha watu zaidi ya 20 kujeruhiwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako