• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika Mashariki zakutana Khartoum ili kuhimiza mchakato wa amani Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-08-10 09:36:12

    Jumuiya ya Maendeleo ya Serikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD imefanya kongamano maalumu la mawaziri huko Khartoum ili kuhimiza mchakato wa amani Sudan Kusini.

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Bw. Al-Dirdiri Ahmed kwenye ufunguzi wa mkutano huo amesema, mkutano huo unalenga kutoa moyo mpya kwa mazungumzo kuhusu Sudan Kusini na kutunga ratiba ya utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa Agosti 5 na pande husika za mapambano.

    Ameeleza kuwa kutokana na moyo mpya, wanaamaini kanda hiyo itaungana ili amani ifikiwe nchini Sudan Kusini.

    Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Bw. Hirut Zemene amesema, kusainiwa kwa makubaliano hayo kuhusu mgawanyo wa madaraka na uratibu wa usalama kwa makundi hasimu nchini Sudan Kusini, kumeonesha uwezo wa nchi za Afrika kutatua masuala yao chini ya mfumo wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako