• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • DRC yaanza kazi ya kutoa chanjo ili kukabiliana na mlipuko mpya wa Ebola

    (GMT+08:00) 2018-08-10 10:13:55

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC imeanza kazi ya kutoachanjo ili kukabailiana na duru mpya ya mlipuko wa Ebola katika jimbo la Kivu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

    Kwa mujibu wa WHO, hivi sasa DRC ina dozi 3220 za chanjo ambayo ufanisi wake umethibitishwa katika matumizi ya majaribio ya zamani. Watu wa kwanza kupatiwa chanjo hiyo ni wahudumu wa afya, watu waliogusana na wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa Ebola na wale waliowasiliana nao.

    Wakati huohuo, Umoja wa Afrika umepongeza maendeleo ya mchakato wa uchaguzi wa urais na wabunge wa DRC ambao umemaliza kazi ya kuandikisha wagombea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako