• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kamisheni ya Afya ya China yakanusha tuhuma za kutolewa chanjo zilizopitwa na wakati

  (GMT+08:00) 2018-08-10 16:06:13

  Kamisheni ya Afya ya China NHC imesema chanjo zilizotajwa kwenye ripoti za mtandaoni kuwa zilitolewa baada ya kupitwa na wakati katika mji wa Shangluo mkoani Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China zimethibitishwa kuwa ziko ndani ya muda wake wa matumizi.

  Kamisheni hiyo imesema, ripoti zilizotolewa kwenye mtandao wa internet zinajumuisha aina tano za chanjo zikiwemo za kinga dhidi ya DPT, ECM, na MMR, ambazo zilitolewa katika kliniki tatu za chanjo mjini humo, ambazo pia ziligunduliwa kuwa na wafanyakazi wachache, vifaa visivyo na ubora na uongozi mbaya.

  Taarifa iliyotolewa na kamisheni hiyo imesema, wafanyakazi wa kliniki hizo walikosea kuandika namba sahihi kwenye hati za chanjo zilizotolewa kwa watu waliopewa chanjo hizo, na kuzusha tuhuma.

  Timu ya uchunguzi imeitaka serikali ya mkoa kuandaa mipango ya kufanya ukarabati, kufanya ukaguzi na usimamizi katika vituo vya kutoa chanjo, na kuziba mapengo katika usimamizi wa utoaji wa chanjo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako