• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mtu wa kumi athibitishwa kufa kwa Ebola mashariki mwa DRC

  (GMT+08:00) 2018-08-10 16:57:50
  Wizara ya afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imesema mtu wa 10 aliyethibitishwa kuambukizwa homa ya Ebola amefariki jana mkoani Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo.

  Waziri wa afya wa nchi hiyo Bw. Oly Ilunga amesema mlipuko wa kumi wa homa ya Ebola umetangazwa, na virusi vya Ebola vimeenea kwenye maeneo ya misitu ya ikweta nchini humo.

  Ugonjwa huo ambao, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kumalizika nchini humo mwezi uliopita, umerejea tena na kesi ya kwanza kuthibitishwa mjini Beni Agosti Mosi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako