• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Asilimia 60 ni mstari mwekundu uliochorwa na Marekani kwa washindani wake

  (GMT+08:00) 2018-08-10 19:07:18

  Wiki hii Marekani na China zimeamua kutozana ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 16 za kimarekani kutoka upande mwingine kuanzia tarehe 23 mwezi huu. Hii inaashiria kuanza rasmi kwa duru ya kwanza ya vita ya biashara iliyoanzishwa na Marekani, inayohusisha bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 50 za pande hizo mbili. Sera ya ushuru ya Marekani dhidi ya China inaonekana kuwa inalenga kutatua suala la "biashara zisizo za haki" kati ya pande hizo mbili, lakini kwa undani, lengo lake halisi ni kuzuia mshindani wake anayeibuka kwa kasi, ili kuendelea kulinda hadhi yake, kuongoza utaratibu wa pande nyingi na kujipatia maslahi makubwa ya kiuchumi.

  Katika historia ya Marekani ya miaka 200 tu, nchi hiyo ilitumia mbinu hiyo mara mbili kukandamiza washindani wake waliofikia asilimia 60 ya pato lake la ndani GDP, kwanza ni Russia, na pili ni Japan.

  Historia hiyo inathibitisha kuwa, asilimia 60 ni mstari mwekundu uliochorwa na Marekani kwa washindani wake, nchi yoyote itakayovuka mstari huo, Marekani itaichukulia hatua bila kujali ikitadi yake au mfumo wake wa siasa.

  Lakini China ya leo sio Russia, wala sio Japan ya wakati huo. Kwanza, China ina soko kubwa la matumizi na majukwaa mapya ya ushirikiano ikiwemo "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Japan ya miaka 90 ya karne iliyopita ilikuwa inategemea sana uuzaji nje, haswa kwenye masoko ya Ulaya na Marekani. Takwimu zinaonesha, katika miezi saba iliyopita, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi za Ukanda Mmoja, Njia Moja imefikia dola za kimarekani bilioni 668, ikiwa ni zaidi ya asilimia 27 ya biashara ya jumla ya China kwa nje. Pili, China ina mfumo imara wa kisiasa na mkakati wa maendeleo wa muda mrefu, ambavyo Japan haikuwa navyo wakati huo. Tatu, China ina mfumo kamili na mkubwa zaidi wa viwanda duniani, na imechukua nafasi muhimu kwenye mnyororo wa utengenezaji bidhaa kote duniani, hadhi ambayo kama Marekani inajaribu kuiyumbusha pia itajihujumu kiuchumi.

  China na Japan zote zilikandamizwa na Marekani kwa mbinu zinazofanana na katika wakati unaofanana, lakini hatma zao zitakuwa ni tofauti. Msingi wa maendeleo ya China hautayumbishwa, na China itaendelea kusonga mbele kwa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako