• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaweka mkazo kutuliza hali ya ajira

  (GMT+08:00) 2018-08-10 19:19:51

  Mkutano wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China umetoa kipaumbele kutuliza hali ya ajira katika kazi ya uchumi ya nusu ya pili ya mwaka huu. Mkutano huo kwa mara ya kwanza umetoa agizo ya kutuliza hali ya ajira, mambo ya fedha, biashara ya kimataifa, uwekezaji kutoka nje, na matarajio ya ongezeko la uchumi, kuonyesha ishara ya kuhimiza maendeleo yenye sifa bora ya uchumi kwa madhubuti.

  Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, China imetimiza watu wa mijini zaidi milioni 7.52 kupata ajira, idadi ambayo imeongezeka kwa laki 1.7 kuliko mwaka jana wakati kama huo, muundo wa ajira umeboreshwa zaidi, kiwango cha mshahara kimeongezeka na kiasi cha ukosefu wa ajira kimedumisha kiwango cha chini. Ingawa hali ya ajira imeendelea vizuri katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, lakini kutokana na mageuzi ya muundo wa uchumi wa China na kupandishwa kwa mgogoro wa kibiashara, ni muhimu kwa hali ya ajira kutuliza uchumi.

  Mkutano wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China uliofanyika hivi karibuni umepanga kazi ya uchumi katika nusu ya pili ya mwaka huu, na kutoa kipaumbele katika kutuliza hali ya ajira. Idara mbalimbali za serikali pia zimeshirikiana na kutoa hatua 10 za kutuliza na kuhimiza upatikanaji wa ajira.

  Ofisa wa idara ya ajira ya kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Ha Zengyou amesema hatua hizo ni pamoja na kuendeleza nguvu mpya za kuhimiza ongezeko la uchumi, kuhimiza mageuzi ya viwanda vya jadi, kuharakisha mageuzi ya muundo wa kilimo, kuunga mkono wakulima wanaofanya kazi mjini kurudi vijijini kuanzisha biashara, kupanua sekta za ajira kwa nguvukazi vijijini.

  "ni lazima kuboresha muundo wa masomo katika vyuo vikuu, kuimarisha nguvu mpya za kuhimiza ongezeko la uchumi, kuongeza nafasi nyingi zaidi zenye sifa bora zinazofaa wahitimu wa vyuo vikuu na watu wenye ustadi wa juu. Vilevile kuendeleza kwa nguvu kubwa ajira za huduma zinazohusu maisha ya watu, kama vile kazi za nyumbani na huduma kwa wazee. Pia ni lazima kufanya uvumbuzi katika njia za usimamizi, na kuendelea kuendeleza sekta zinazojitokeza, ili kuongeza ajira kutokana nguvu mpya ya kuhimiza uchumi."

  Habari nyingine zinasema, China itapunguza zaidi gharama za matumizi ya wafanyakazi, itahimiza viwanda kulinda ajira zilizopo sasa, na kuimarisha uwezo wa kukabiliana hatari ya ukosefu wa ajira.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako