• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zaidi ya Sh10M za walipa kodi zapotea baada ya ripoti ya sukari kutupwa

  (GMT+08:00) 2018-08-10 19:26:24

  Wakenya walipoteza zaidi ya Sh10 milioni kwa kipindi cha mwezi mmoja, pesa ambazo zililipwa wabunge wanachama wa kamati iliyochunguza sakata ya uingizwaji nchini wa sukari ya magendo, kama marupurupu ya kuhudhuria vikao. Hii ni baada ya wabunge kutupilia mbali ripoti ya kamati hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Kieni Kanini Kega na mwenzake wa Mandera Kusini Adan Haji wakidai kamati hiyo ilishindwa kutegua kitendawili cha iwapo kuna sukari yenye sumu nchini au la.

  Kiwango hicho cha fedha hakijumuishi gharama ya usafiri, malazi na chakula ambayo wabunge hao 38 walitumia walipozuri maeneo mbalimbali kukagua sheheni za sukari zilizoingizwa nchini kinyume cha sheria.

  Aidha, kiasi hicho cha fedha (Sh10 milioni) hazijajumuisha pesa ambazo zililipwa wafanyakazi wa bunge kama makarani na walinzi walitoa huduma mbalimbali kwa kamati hiyo iliyojumuisha wanachama wa kamati za Kilimo na Biashara. Kwa mujibu wa mwongozo wa Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) kuhusu marupurupu ya wabunge, wenyeviti wa kamati hupokea Sh12,000 kwa kila kikao huku wanaibu wao wakupata Sh7,000. Na wanachama wa kawaida hutia kibindoni Sh5,000.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako