• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yakataa sukari kutoka Uganda kuingizwa nchini humo

  (GMT+08:00) 2018-08-10 19:26:42

  Rais John Magufuli ametaja sababu za kuzuiwa sukari kuingia nchini humo kuwa baadhi ya watu huleta sukari isiyozalishwa nchini Uganda.

  Februari mwaka huu, rais Yoweri Museveni wa Uganda alimraia Magufuli kuwahimiza wafanyabiashara wa Tanzania kununua kwa wingi sukari kutoka Taifa hilo kwa sababu ipo ya kutosha na ziada.

  Museveni alisema Taifa hilo limekuwa likizalisha ziada ya sukari, hivyo itakuwa vyema iwapo wafanyabiashara wa Tanzania watachangamkia fursa hiyo.

  Rais Magufuli alikubaliana na wazo hilo na kusema litasaidia kukabiliana na changamoto ya upungufu wa sukari nchini mwake.

  Hata hivyo, hivi karibuni Tanzania ilisimamisha uingizaji wa sukari kutoka Uganda, jambo lililoibua malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wa nchi hiyo.

  Dk Magufuli akizungumza amesema Serikali ililazimika kusitisha uigizaji wa sukari baada ya kubaini kiwango kikubwa hakizalishwi Uganda.

  Rais alisema baadhi ya wafanyabiashara kutoka nje ya Uganda walikuwa wakipenyeza sukari nchini humo na baadaye kuisafirisha hadi Tanzania, jambo alilosema ni hatari kwa viwanda vya ndani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako