• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Duka la Nakumatt Ukay labomolewa

  (GMT+08:00) 2018-08-10 19:27:02

  Duka la Nakumatt Ukay lililopo mtaani Westlands jijini Nairobi limebomolewa. Matingatinga matatu yanayoendesha shughuli hiyo yaliamkia ubomoaji wa duka hilo, chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa polisi, wale shirika la huduma ya vijana kwa taifa (NYS) na wa Halmashauri ya Mazingira (Nema).

  Hata hivyo, tingatinga moja liliangukiwa na sehemu ya jumba lililokuwa likibomolewa na kulazimu shughuli hiyo kusitishwa kwa muda mfupi kabla ya kuendelea. Shughuli hiyo inaendelea siku moja tu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kusisitiza kuwa ubomoaji wa majengo haramu unaofanyika jijini Nairobi utaendelea.

  Kenyatta amesema kwamba ubomoaji huo utafanyika katika miji mingine, kwa majumba ambayo hayakuzingatia sheria za ujenzi hasa yaliyojengwa kwa ardhi iliyotengewa upanuzi wa miundo msingi kama barabara.

  Ubomoaji huo ulioanza Jumatatu unaendelea kwa majengo yanayolengwa na serikali, licha ya wamiliki kwenda kortini wakitaka shughuli isimamishwe. Jumanne, jumba la kibiashara la Southend Mall lililokuwa katika barabara ya Lang'ata pia lilibomolewa, Nema ikishikilia kuwa lilijengwa karibu sana na Mto Ngong kinyume na sheria na hivyo kuhatarisha mazingira.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako