• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 16 wauawa katika shambulizi lililofanywa na kundi la Taliban nchini Afghanistan

  (GMT+08:00) 2018-08-10 19:32:09

  Watu 16 wameuawa na wengine 33 kujeruhiwa baada ya wapiganaji wa kundi la Taliban kufanya shambulizi kubwa mjini Ghazni, mkoa wa Ghazni, mashariki mwa Afghanistan mapema leo.

  Mkuu wa jeshi la polisi mkoani humo Farid Ahmad Mashal amesema shambulizi hilo limetokea leo asubuhi baada ya mamia ya wapiganaji wa kundi la Taliban kuvamia majengo ya taasisi muhimu za serikali ikiwemo idara ya polisi, kurugenzi ya usalama wa taifa na ofisi ya mkuu wa mkoa.

  Kundi la Taliban halijatoa tamko lolote kuhusiana na tukio hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako