• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tahadhari kubwa yatolewa nchini Tanzania baada ya ugonjwa wa Ebola kutokea tena nchini DRC

    (GMT+08:00) 2018-08-11 17:12:01

    Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Bi. Ummy Mwalimu amesema taifa hilo lilitoa tahadhari ya juu zaidi baada ya ripoti za kutokea tena kwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

    Waziri huyo alisema mjini Dar es Salaam kuwa watu wangekuwa katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo hasa wale wanaogusana na watu kutoka DRC, hivyo inawapasa watanzania kuchukua tahadhari kubwa ili kujizuia kupata ugonjwa huo.

    Akisema wizara yake ilitoa tahadhari hiyo hasa kwa wale wanaoishi kwenye mikoa inayopakana na nchi za DRC, Uganda na Rwanda, ambayo ni Mwanza, Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa na Songwe.

    Aidha waziri huyo alisema hakuna maambukizi ya Ebola nchini Tanzania tangu ugonjwa huo ugunduliwe katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC.

    Juma lililopita , wizara ya afya ya DRC ilitangaza kutokea kwa mara ya pili kwa ugonjwa wa Ebola ambapo jumla ya watu 44 waliripotiwa kuambukizwa, na 17 wakiwa wamethibitishwa kuwa nao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako