• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatarajia dola milioni 400 kutokana na mauzo ya hisa zake, kusaidia bajeti

    (GMT+08:00) 2018-08-11 17:40:12

    Kenya inataka kukusanya dola za kimarekani milioni 400 kwa mwezi huu kupitia mauzo ya hisa zake ili zisaidie utekelezaji wa bajeti.

    Pesa hizo zitatokana na hisa ilizowekeza katika kipindi cha miaka 10 zikiwa na thamani iliyotokana na bei ya uuzaji wa hisa hizo iliyotangazwa na benki kuu.

    Wawekezaji wataanza rasmi kutoa zabuni Agosti 10 na benki hiyo itafanya mnada Agosti 20.

    Mwezi uliopita serikali ya Kenya ilitangaza mauzo ya hisa zake za miaka 20 zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 400 ili kusaidia bajeti lakini hayakuwa na ufanisi, ambapo mauzo ya jumla yalikuwa asilimia 35 tu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako