• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Ethiopia asema vurugu zilizotokea mashariki mwa nchi hiyo zimedhibitiwa

    (GMT+08:00) 2018-08-12 16:17:11

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed amevunja ukimya wa wiki nzima na kutangaza kwamba vurugu zilizotokea juma lililopita kwenye jimbo la Somali nchini humo, kwa sasa zimedhibitiwa.

    Akizungumza na vyombo vya habari, Bw. Ahmed amesema eneo hilo sasa linarejea katika hali ya kawaida kutokana na msaada wa serikali kuu ya Ethiopia na maafisa kutoka uongozi wa mkoa.

    Pia amesema majadiliano yanaendelea kwa sasa kati ya serikali na maofisa wa jimbo hilo ili kuzuia kutokea tena kwa vurugu ambazo tayari zimeua idadi kubwa ya watu isiyojulikana na wengine wakijeruhiwa.

    Baadhi ya miji katika jimbo hilo iligeuka na kuwa eneo la vurugu mbaya zilizopelekea vifo mwishoni mwa juma lililopita baada ya tarehe 4 Agosti wanajeshi kupelekwa katika jiji la Jijica ambapo ni makao makuu ya jimbo la Somali ili kuwakamata viongozi wa ngazi za juu wa jimbo hilo akiwemo Abdi Omar Mohammed ambaye ni Rais wa Jimbo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako