• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yagundua bandari haramu, na viwanja vya ndege vinavyotumika kusafirisha bidhaa za magendo

    (GMT+08:00) 2018-08-12 16:39:05

    Mamlaka nchini Tanzania zimetambua bandari haramu 134 na viwanja 58 vya ndege visivyosajiliwa ambavyo vinatumika kusafirisha bidhaa za magendo, na kuisababishia serikali hasara kubwa ya mapato.

    Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania Bw. Isaac Kamwelwe amegundua idadi kubwa ya bandari haramu na viwanja hivyo vya ndege wakati akifanya ziara ya kuifahamu Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na bandari ya Dar es Salaam.

    Amesema ukaguzi uliofanywa na TPA imefichua bandari 134 haramu kwenye pwani ya maziwa na pwani ya Bahari ya Hindi, na viwanja 58 vya ndege vylivyopo sehemu tofauti ya nchi vikibainika kuwa vinatumika bila ya kusajiliwa.

    Waziri huyo alitaja baadhi ya bidhaa zinazoingizwa nchini humo kwa njia ya magendo kupitia njia hizo kuwa ni sukari, mafuta ya kupikia, saruji, mbao, madini na bidhaa nyingine nyingi ambazo zimechangia kuathirika kwa maendeleo ya viwanda vya ndani.

    Akisema serikali kwa sasa inafanya mapitio ya sheria ili njia hizo haramu ziweze kuwekwe kwenye mwavuli mmoja ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako