• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasayansi waunda chandarua ambacho ni silaha mpya ya kupambana na malaria

    (GMT+08:00) 2018-08-12 16:56:55

    Chandarua kilichoundwa kwa ajili ya kuua mbu kinaweza kuzuia mamilioni ya vifo vitokanavyo na malaria katika eneo la kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika, hii ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti mpya yaliyochapishwa ijumaa kwenye jarida moja linalohusu masuala ya afya liitwalo The Lancet.

    Majaribio ya matibabu yaliyofanywa kwa miaka miwili nchini Burkina Faso yameonyesha kuwa vyandarua vyenye mchanganyiko wa kemikali vimesababisha kupungua kwa asilimia 12 kwa wagonjwa wa malaria, ikilinganishwa na vyandarua vya kawaida.

    Wakati wa majaribio hayo yaliyofanyika kwenye maeneo 40 ya huko Burkina Faso yakijumuisha vijiji 91 na watoto 1,980 mwaka 2014, na watoto 2,157 mwaka 2015 na wote wakiwa ni wenye umri wa kuanzia miezi sita hadi miaka mitano, vyandarua vya kawaida viliondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na vyandarua vilivyowekwa mchanganyiko wa dawa aina ya Pyrethroid na Pyriproxyfen.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako