• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaishukuru China kwa kutoa udhamini wa masomo ya udaktari

    (GMT+08:00) 2018-08-13 09:21:08

    Tanzania imeishukuru China kwa kutoa udhamini wa masomo ya udaktari na mafunzo mafupi kwa wafanyakazi wa afya wa Tanzania.

    Akiongea kwenye sherehe fupi ya kuwaaga wanafunzi wa Tanzania wanaokuja China kwa mafunzo, waziri wa elimu, sayansi na teknolojia wa Tanzania Prof. Joyce Ndalichako, amesema China imethibitisha kuwa rafiki mzuri wa Tanzania kutoa uungaji mkono kwenye sekta mbalimbali, na udhamini kwa wanafunzi wa udaktari wa China ni mfano wa juhudi za China katika kuisaidia Tanzania kuendeleza elimu na raslimali watu.

    Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Wang Ke, amesema ushirikiano kati ya China na Tanzania kwenye sekta ya afya ulianza mwaka 1964, wakati China ilipoanza kutuma vikundi vya madaktari nchini Tanzania. Mpaka sasa watu milioni 22 wametibiwa na madaktari wa China, na sasa wachina 32 wanafanya kazi katika hospitali mbalimbali za Tanzania bara na Tanzania Zanzibar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako