• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yatoa mwito wa kufikisha misaada kwa uhuru na usalama kwenye maeneo yaliyokumbwa na Ebola DRC

    (GMT+08:00) 2018-08-13 09:21:29

    Shirika la Afya duniani WHO limetoa mwito wa kuwepo kwa njia huru na salama ya kufikisha misaada kwenye eneo lililokumbwa na mlipuko wa Ebola, baada ya ugonjwa huo kulikumba kwa mara ya kwanza eneo lenye watu wengi linaloathiriwa na mgogoro nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Wiki moja baada ya serikali ya nchi hiyo kutangaza mlipuko mwingine wa Ebola, mkurugenzi wa WHO Dr. Tedros Ghebreyesus, mkurugenzi wa Shirika hilo kanda ya Afrika Dk. Matshidiso Moeti, na Mkurugenzi wa mambo ya dharura Dk. Peter Salama, wamefanya ziara ya siku mbili katika jimbo la Kivu kaskazini karibu na eneo la kiini cha mlipuko wa sasa.

    Eneo hilo kwa sasa linakumbwa na mapigano, hali inayoleta changamoto kwa vikundi vya madaktari kwenda maeneo ya ndani kwenye jamii, kutafuta watu walioathiriwa, na kuwapima mara mbili kwa wiki kwa muda wa wiki tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako