• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yakanusha kuwa Saudi Arabia imezuia uagizaji wa kondoo

    (GMT+08:00) 2018-08-13 09:21:49

    Wizara ya mifugo ya Sudan, imekanusha habari kuwa mamlaka nchini Saudi Arabia zimesimamishwa uagizaji wa kondoo kutoka Sudan.

    Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema, serikali ya Sudan inafuata kanuni za afya ya wanyama kwa mujibu wa vigezo vya kimataifa kwenye mambo ya chanjo na karantini, na pia inazingatia masharti yaliyofikiwa na wauzaji nje.

    Wizara hiyo imekanusha ripoti za vyombo vya habari kuwa marufuku hiyo imetolewa siku mbili zilizopita, na meli zilizokuwa na kondoo kutoka Sudan zimerudishwa.

    Taarifa imesema hakuna meli iliyorudishwa na wanyama kutoka Sudan, na hawajapata barua yoyote kutoka Saudi Arabia kuhusiana na jambo hilo. Wizara imesema habari za uongo kama hiyo, zina lengo la kudhuru uchumi wa Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako