• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la waasi la Ethiopia ONLF latangaza usitishaji vita wa upande mmoja

    (GMT+08:00) 2018-08-13 09:28:21

    Kundi la waasi la Ethiopia Ogaden National Liberation Front ONLF lililoko katika jimbo la Somali nchini Ethiopia, limetangaza kusitisha vita kwa muda.

    Taarifa iliyotolewa na kundi hilo imesema hatua ya kundi hilo inalenga kuweka msingi wa mazungumzo ya amani yatakayofuata, ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kutuliza manung'uniko katika eneo hilo.

    Taarifa imesisitiza kuwa amani inahitajika sana kwa kundi la ONLF, serikali ya jimbo la Somali na pande nyingine husika katika kukomesha mapambano yaliyodumu kwa muda mrefu katika jimbo hilo.

    Kundi la ONLF limetangaza kuwa kuanzia jana litasimamisha operesheni zote za kijeshi hadi makubaliano ya kusitisha vita na serikali ya Ethiopia yatakapofikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako