• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya aahidi kutokomeza ufisadi na vitendo vya kufumbia macho uhalifu nchini humo

    (GMT+08:00) 2018-08-13 10:03:50

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameahidi kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi na vitendo vya kufumbia macho watenda makosa.

    Bw. Kenyatta amesema, ataendelea kazi ya kurudisha tena mali za umma zilizopatikana kwa njia haramu ikiwemo ardhi. Pia amesema, ingawa amepata maombi ya kusimamisha bomoa bomoa ya majengo ya pembezoni mwa Nairobi, lakini kazi hiyo itaendelea kutekelezwa, ambayo imeonesha nia thabiti ya serikali ya kutokomeza hali ya kutoadhibiwa kwa watenda makosa na kurejesha utawala wa sheria.

    Bw. Kenyatta amesema, fedha na uhusiano wa kisiasa hautawanusuru wale waliofanya makosa.

    Serikali ya Kenya imekuwa inaendelea na mapambano dhidi ya ufisadi, na kubomoa majengio yaliyojengwa karibu na mto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako