• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mbio za Baiskeli, Rwanda: Samuel Mugisha wa Rwanda ashinda ubingwa wa mashindano ya Rwanda

  (GMT+08:00) 2018-08-13 10:09:12

  Samuel Mugisha wa Rwanda ameshinda ubingwa wa mashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli ya Rwanda (Tour Du Rwanda) kwa mwaka huu, baada ya kurekodi muda mfupi zaidi kuliko waendesha baiskeli wengine katika mashindano hayo yaliyodumu kwa siku 8.

  Rekodi inaonyesha kuwa, Samuel ametumia jumla ya saa 24 dakika 26 na sekunde 53 katika mzunguko wote wa mbio hizo zenye umbali wa jumla wa kilomita 953.2, na mshindi wa pili ni Jean Claude Uwizeye wa Rwanda na Nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mulu HaileMichael wa Ethiopia.

  Licha kupata zawadi ya ubingwa wa jumla, Mugisha pia amepata tuzo nyingine za umahiri, zikiwemo mwendesha baiskeli bora, mwendesha baiskeli bora chipukizi, mwendesha baiskeli bora kutoka Afrika na mwendesha baiskeli bora kutoka Rwanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako