• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpira wa Pete (Netball) Wanawake: Mashindano ya ubingwa wa Afrika kuanza leo nchini Zambia

    (GMT+08:00) 2018-08-13 10:10:39

    Timu za mpira wa pete (netball) za Kenya, Uganda, Malawi, Namibia, Zimbabwe na Botswana na wenyeji Zambia leo zinatarajiwa kuanza mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika.

    Kenya ambao wanashiriki mashindano ngazi ya bara ikiwa ni baada ya miaka 7 kupita tangu walipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 2011 kwenye mashindano ya All Africa Games nchini Swaziland, tayari wamewasili jana mjini Lusaka wakiwa na kikosi cha wachezaji 14.

    Licha ya kujipatia zawadi za ushindi wa mashindano hayo, bingwa pamoja na mshindi wa pili watafuzu moja kwa moja kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia inayotarajiwa kufanyika mwezi jula mwaka 2019 nchini Uingereza.

    Afrika Kusini na Malawi tayari zimekwishafuzu kwa ajili ya kombe la Dunia kutokana na viwango vyake vya ubora kwenye mchezo huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako