• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tennis, Canada: Nadal ashinda ubingwa wa Rogers Cup

    (GMT+08:00) 2018-08-13 10:10:57

    Rafael Nadal wa Hispania jana ameshinda taji la ubingwa wa mashindano ya tennis ya Canada na kuzima ndoto za chipukizi Stephano Tsitsipas wa Canada aliyekuwa na matumaini makubwa ya kushinda ambapo jana ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.

    Licha ya kukabiliwa na upinzani kutoka Tsitsipas, Nadal alifanikiwa kushinda mechi hiyo kwa seti ya alama 6-2 7-6 7-4.

    Matumaini ya ubingwa kwa Tsitsipas yalikuja baada ya chipukizi huyo kupata ushindi kwenye mechi za awali dhidi ya nyota wakubwa wa mchezo huo duniani wakiwemo Dominic Thiem wa Austria, Novak Djokovic wa Serbia na Alexander Zverev wa Ujerumani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako