• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Cristiano Ronaldo afunga goli la kwanza katika mechi ya kwanza Juve

    (GMT+08:00) 2018-08-13 10:11:16

    Mchezaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo jana amefunga goli lake la kwanza katika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na klabu ya Juventus ya Italia.

    Ronaldo alifunga goli hilo kunako dakika ya 8 kwenye mechi dhidi ya kikosi B cha timu hiyo iliyopigwa kwenye makazi ya wamiliki wa timu hiyo ya Villar Perosa kaskazini ya Italia kama ilivyo desturi kila inapofika wakati wa kuelekea msimu mpya wa ligi kuu nchini Italia.

    Kikosi A cha Juventus kilipata ushindi wa magoli 5-0 kwenye mechi hiyo ambayo hata hivyo haikuisha kwani katika dakika ya 72 ilikatishwa baada ya mashabiki kuuvamia uwanja ili kujaribu kumlaki Ronaldo ambaye wanaamini kuwa atawaletea makombe ya ubingwa msimu huu, jambo ambalo wengi walifanikiwa kupiga naye picha na akisaini kumbukumbu zao za kimichezo.

    Hiyo ilikuwa ni mechi ya kwanza ya Ronaldo tangu ajiunge na Juventus mwezi uliopita na akitarajiwa kucheza mechi ya kwanza ya ligi kuu timu hiyo itakapokutana na Chievo jumamosi ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako