• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakimbizi 150 wa Syria warudi nyumbani kutoka Lebanon

    (GMT+08:00) 2018-08-13 19:44:13

    Gazeti la kwenye mtandao la Elnashra nchini Lebanon limeripoti kwamba wakimbizi 150 wa Syria wamerudi nchini mwao, na kufanya idadi ya wakimbizi waliorejea kwao kutoka Shabaa, Lebanon kufikia 1,000 katika miezi miwili iliyopita.

    Ofisi ya Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) nchini Lebanon imesema, wakimbizi zaidi ya milioni moja wa Syria wameandikishwa, na serikali ya Lebanon inakadiria kuwa idadi kamili ya wakimbizi wa Syria nchini humo inafikia milioni 1.5.

    Mwezi uliopita, Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ziliandaa mkakati wa kuhakikisha usalama wa wakimbizi wa Syria wanaorejea nchini mwao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako