• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wazee wa Afrika watajwa kuathiriwa zaidi na misukosuko ya kibinadamu

    (GMT+08:00) 2018-08-14 09:07:27

    Utafiti kuhusu wakimbizi wazee barani Afrika umeonesha kuwa wazee wa kanda ya pembe ya Afrika wameathiriwa zaidi na misukosuko ya kibinadamu iliyosababishwa na migogoro na majanga ya asili, kutokana na kutokuwepo taratibu na juhudi za kutosha za kuwasaidia.

    Ripoti ya utafiti huo uliofanywa na Shirika la hisani la HelpAge International nchini Kenya, Sudan, Ethiopia na Uganda, inasema wazee wenye ulemavu walipewa msaada mdogo kutoka kwa familia zao wakiwa ukimbizini, kwa kuwa raslimali zilikuwa chache na familia zilichoka kuwatunza.

    Ripoti inasema migogoro na majanga ya asili yanayotokea mara kwa mara katika eneo la Afrika Mashariki vimeharibu mfumo wa kijamii na kudhoofisha hadhi ya wazee ya kuwa na ushawishi na heshima kwenye jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako