• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaongeza akiba ya kimkakati ya chakula

    (GMT+08:00) 2018-08-14 09:07:45

    Kenya imesema inapanga kuongeza akiba ya kimkakati ya chakula hadi kuwa magunia milioni 8 ya mahindi kwa kipindi cha muda wa kati, ili kuimarisha usalama cha chakula. Waziri wa ugatuzi Bw. Eugene Wamalwa amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa dola milioni 14 za kimarekani zimetengwa mwaka huu kununua mahindi ili kuongeza akiba ya chakula ya sasa ya magunia milioni 3, kiasi ambacho amesema hakitoshi kukabiliana na maafa ya asili. Takwimu za wizara ya kilimo ya Kenya zinasema Kenya inazalisha magunia milioni 39 ya mahindi kila mwaka, ikilinganishwa mahitaji ya magunia milioni 46.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako