• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Ethiopia apongeza mchango wa China katika maendeleo ya viwanda

    (GMT+08:00) 2018-08-14 09:17:10

    Rais Mulatu Teshome wa Ethiopia amepongeza mchango wa China katika maendeleo ya viwanda nchini Ethiopia, na kuisadia nchini hiyo kwa kuonyesha kuwa, katika miaka kumi ijayo usimamizi na mipango sahihi, vitaifanya Ethiopia ibadilike kutoka nchi ya uchumi unaotegemea sekta ya kilimo, na kuwa nchi ya uchumi unaotegemea viwanda.

    Akiongea baada ya kutembelea eneo la viwanda la mashariki mwa nchi hiyo lililojengwa na China, Rais Teshome amesema miaka kumi iliyopita, eneo hilo lilikuwa ni eneo la kilimo tu, lakini kutokana na juhudi eneo hilo limekuwa eneo la kiwango cha juu kwenye sekta ya viwanda, likiwa na viwanda vya dawa, karatasi na nguo.

    Balozi wa China nchini Ethiopia Bw. Tian Jian, aliyeambatana Rais Theshome kwenye ziara yake amesema uhusiano kati ya China na Ethiopia, ni mfano wa kuigwa wa uhusiano wa kusini-kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako