• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Riadha: Mwanariadha Mazuronak atwaa dhahabu

    (GMT+08:00) 2018-08-14 10:34:49

    Mwanariadha Volha Mazuronak wa Belarus juzi ametwaa medali ya dhahabu katika mbio za marathoni za ubingwa wa ulaya 2018 kwa upande wa wanawake licha ya kukumbwa na kadhia ya kutokwa damu nyingi puani.

    Mshindi wa pili katika mbio hizo zilizofanyika mjini Berlin nchini Ujerumani alikuwa ni Clemence Clavin wa Ufaransa na Eva Nyvltova wa Jamhuri ya Czech akishika nafasi ya tatu.

    Kwa upande wa wanaume Koen Naert wa Ubelgiji alishinda nafasi ya kwanza, Tadesse Abraham raia wa Uswisi mwenye asili ya Ethiopia alishinda nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikitwaliwa na Yassine Rachik wa Italia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako