• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda :Uzalishaji wa kahawa maalum Rwanda wafikia asilimia 58

    (GMT+08:00) 2018-08-14 20:00:54

    Uzalishaji wa kahawa maalum nchini Rwanda umeongezeka hadi asilimia 58 mwaka 2017 na unatarajiwa kukua hadi asilimia 80 mwaka 2020.

    Hii ni kulingana na takwimu za Bodi ya Taifa ya Maendeleo ya Kilimo (NAEB).

    Kahawa maalum ni ile inayodumisha ubora kutoka kwenye shamba hadi kwenye mteja wa mwisho na inapata alama zaidi ya 80 kati ya 100.

    Ili kufaniukisha hilo, vyombo vyote vinavyohusika katika mchakato wa kuongeza thamani ya kahawa , ikiwa ni pamoja na wakulima na vituo vya kuosha kahawa, vinapaswa kufikia viwango fulani.

    Mkuu wa kitengo cha kahawa kwenye bodi ya NAEB, Celestin Gatarayiha amesema bei ya wastani ya kahawa maalum kutoka Rwanda ni dola 4 ikilinganishwa na dola 2 kwa kahawa isiyo maalum.

    Hata hivyo, aliongeza kuwa kuna wauzaji wengine wanaweza kupata hadi dola 8 kwa kahawa maalum kulingana na soko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako