• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria: Benki ya Dunia yaidhinisha mkopo wa dola bilioni 2.1 kwa Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-08-14 20:01:38

    Benki ya Dunia imeidhinisha mkopo wa dola bilioni 2.1 kwa Nigeria za kusaidia miradi mbalimbali nchini humo.

    Mkopo huo utatumika kufadhili miradi saba katika sekta muhimu nchini.

    Benki ya Dunia, katika taarifa iliyoorodheshwa miradi hiyo saba ambayo ni pamoja na lishe, upatikanaji wa umeme, uwazi wa fedha, kukabili polio na uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake.

    Benki hiyo hivi karibuni ilipanua Mkakati wa Ushirikiano na Nigeria hadi Juni 30, 2019. Katika kipindi cha 2018 na 2019, msaada wake kwa Nigeria unatarajiwa kuzingatia uchanganuzi wa mapato na uhamasishaji, na kushiriki kujenga ukuaji wa uchumi wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako