• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:wakaazi wakabiliwa na uhaba wa saruji

    (GMT+08:00) 2018-08-14 20:01:58

    Wakazi wa Dar es Salaam wameanza kukumbana na uhaba wa saruji ambayo imepanda bei kutoka Sh13,500 hadi Sh18,000 kwa mfuko mmoja wa kilo 50.

    Uchunguzi umebaini kutokuwepo kwa saruji ya kutosha katika maduka ya vifaa vya ujenzi kwenye maeneo ya Mwenge, Tegeta na Buguruni.

    Baadhi ya wateja wanalalamikia uhaba huo wakisema kuwa sasa wanalazimika kununua saruji kwa bei ghali.

    Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage alisema tatizo lilikuwa ni matengenezo ya mitambo ya kuzalishia malighafi za simenti katika viwanda kadhaa, lakini sasa yamekamilika hivyo upatikanaji utarudia katika hali ya kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako