• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Kombe la CAF: Rayon (Rwanda), Gor Mahia(Kenya) na Yanga (Tanzania) zajiandaa kucheza jumapili

  (GMT+08:00) 2018-08-15 11:12:34

  Rayon Sport ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya na Yanga ya Tanzania, zimeendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi za raundi ya tano za hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika CAF kwa msimu huu zitakazopigwa siku ya jumapili.

  Yanga ambayo imepoteza tumaini la kufuzu hatua ya robo fainali kwa kuwa ina pointi moja tu ikiwa na mechi mbili ambazo hata hivyo hazitaisaidia kwa kuwa tayari timu mbili za juu kwenye msimamo wa kundi ambazo ni idadi hitajikwa ili kufuzu zina pointi ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga.

  Timu hiyo iko mkoani Morogoro nchini Tanzania ikitarajiwa kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya kusafiri kwenda Dar es Salaam itakakofanyika mechi dhidi ya USM Algiers kutoka Algeria.

  Lakini mechi nyingine ya kundi hilo itafanyika mjini Nairobi nchini Kenya ambapo wenyeji Gor Mahia ambao ni vinara wa kundi hilo kwa kuwa na pointi 8 watawakaribisha Rayon Sport wenye pointi 3 lakini wakiwa na matumaini ya kusonga mbele kutokana na hesabu za kisoka.

  Ushindi ni lazima kwa Rayon katika mechi mbili zilizosalia ili iweze kufuzu robo fainali, kwani itafikisha 9, kukiwa na haja ya timu mojawapo kati ya USM au Gor itakayopoteza katika mechi zake mbili.

  Katika mechi hiyo Rayon watakosa huduma ya wachezaji wao muhimu walioadhibiwa na CAF kwa kile kilichodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu, amabo ni kiungo Yannick Mukunza, mshambuliaji Christ Mbondi na golikipa Nzayisenga.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako